Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuchangia damu katika hospitali zote nchini ili kuweza kusaidia kuondokana na tatizo ambalo limekuwa likiwakabili wananchi.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Vicent Mashinji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amewaomba wafuasi wa chama hicho waliopo nchini kote kuhakikisha kuanzia leo wanaenda kujitolea damu ili kuwasaidi wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

“Zoezi la Uchangiaji wa Damu katika mahospitali nchini kote, linalenga kusaidia kuondokana na tatizo linalowakumba wananchi wengi nchini kwetu, hivyo ninawaomba wanachama wetu kuanzia leo wajitokeze kuanza zoezi hilo,”amesema Dkt. Mashinji

Hata hivyo, ameongeza kuwa Lissu kupelekwa Jijini Nairobi siyo kwamba hawawaamini madaktari wa nyumbani, bali wamehitaji kiongozi huyo aweze kupona haraka akiwa katika mazingira yaliyotulia na yatakayomfanya apumzike kwa amani bila kuweweseka kutokana na tukio lililomtokea.

Kukojoa kitandani ni ugonjwa wa akili
Man City, Man United zapinga usajili 'EPL' kufungwa mapema