Chama cha Demokrasia na Maendeleoa (CHADEMA) kimesema kuwa kinajipanga kukabiliana na kamata kamata inayoendelea ndani ya chama hicho.
Hayo yamesema mapema hii leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa viongozi wengi wa chama hicho wamekuwa wakikamatwa kwa makosa ambayo hayaeleweki.
”Sasa hivi imekuwa kama staili kwa viongozi wa chama chetu kukamatwa kwa maagizo ya wakuu wa mikoa na wilaya karibia nchi nzima, hili kwa sasa inatosha, tunajipanga tuweze kuona namna ya kuweza kuondokana nalo,”amesema Makene.
Hata hivyo, akizungumzia kukamatwa kwa mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee, Makene amekiri kuwa ni kweli mbunge huyo amewekwa ndani kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kwa tuhuma za kutoa lugha ya uchochezi.