Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amepokea ripoti ya tume aliyoiunda kuhakiki mali za chama, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.
Kamati hiyo imefanya kazi kwa miezi mitano ambapo imekusanya, imehakiki na kuchambua taarifa na nyaraka zenye maelezo kuhusu idadi, aina na hali ya mali zinazomilikiwa na kusimamiwa na chama,
Aidha, tume hiyo imeangalia vyanzo vya udhaifu wa mifumo na taratibu za usimamizi wa mali, imekusanya ushauri mbalimbali na kutoa mapendekezo ya mikakati na ushauri wa kusimamia mali za chama.
“CCM imeamua kuchukua hatua hii ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya kupiga vita rushwa na ufisadi, huwezi ukaanza kupiga vita rushwa na ufisadi ndani ya Serikali wakati chama kina rushwa na ufisadi, chama nacho tunataka tukisafishe, mambo ya rushwa na ufisadi yaishe ili Tanzania iende vizuri,”amesema Rais Dkt. Magufuli
-
Polisi wapigwa marufuku kula hadharani, kuweka mikono mfukoni
-
CAG abaini uozo hospitali za umma, mamilioni yapigwa
-
Video: Moto waanza kuwaka kiti cha Mbowe Chadema, Ukweli ulinzi ukuta Mirerani