Aliyekuwa mtangazaji wa zamani wa Radio Free Afrika, ITV, Radio One na baadaye Idhaa ya Kiswahili ya DW, Isack Muyenjwa Gamba ameagwa leo katika viwanja vya Hospitali ya Jeshi Lugola jijini Dar es salaam, tayari mwili wake umesafirishwa kuelekea jijini Mwanza na baadaye Bunda kwaajili ya maziko.

Akisoma taarifa fupi ya marehemu, mtangazaji nguli nchini ambaye amewahi pia kufanya kazi na Gamba, Regina Mziwanda amesema kuwa chanzo cha kifo chake kilichogundulika kwenye uchunguzi wa madaktari nchini Ujerumani kimetajwa kuwa ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo kutokana na shinikizo la damu.

“Baada ya uchunguzi wa hospitali nchini Ujerumani, iligundulika kuwa kifo chake kimesababisahwa na kuvuja kwa damu kwenye ubongo kulikosababishwa na shinikizo la damu,”amesema Regina.

Awali akitoa salamu za mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wanahabari kuendeleza umoja na mshikamano katika nyakati zote na kusema kuwa marehemu Gamba amempa umaarufu nchini Ujerumani, kwani alikuwa akihabarisha kila tukio lilikokuwa likitokea Dar es salaam nchini humo.

 

Video: DataVision yasherehekea miaka 20 ya kuokoa maisha, ajira, kulea vipaji
Mmiliki, Wahariri wa Gazeti la Tanzanite watakiwa kujieleza