Udhalilishaji wa watoto ambao kwa kiasi kikubwa umeripotiwa kufanywa na ndugu zao wa karibu au watu wa karibu walioaminiwa, uliamsha hasira za taifa hususan wiki kadhaa zilizopita na kutua bungeni.
Mjadala huo ulitokana na tukio la kusikitisha la mwalimu wa nidhamu wa shule ya St. Florence Academy, iliyoko Mikocheni jijini Dar e Salaam aliyewadhalilisha watoto wanne wa kike wa darasa la saba katika shule hiyo na kisha kutokomea.
Serikali ilichukua hatua haraka kwa kumsaka mwalimu huyo aliyebatizwa jina la ‘mpapasaji’ kwa lengo la kumchukulia hatua kali za kisheria.
Lakini watoto wengi wa kike na kiume wanakumbwa na dhahma hiyo inayowaondolea utu, kuwanyanyasa na kuwatesa kisaikolojia na kimwili kwa maisha yao yote.
Dar24 imezunguka kona kadhaa za jiji la Dar es Salaam na kuangazia kona hizo na wakaazi wake kuhusu ulinzi wa mtoto.
Angalia makala hii fupi, umlinde mwanao na mwana wa mwenzio usimwache nyuma: