Nyota wa muziki wa R&B na Pop, Chris Brown ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘High End’ akiwa amemshirikisha Future na Young Thug katika wimbo huo.

Video hiyo inaanza kwa angalizo kwamba mtoto chini ya miaka17 anatakiwa kuiangalia video hiyo ikiwa tu yuko chini ya uangalizi wa wazazi au mtu yeyote mzima kutokana na picha za kutisha zinazoonekana katika video hiyo.

Katika video hiyo pia kuna ujumbe unaosema mahudhui na picha zinazoonekana katika video hiyo hazihusiani na kuabudu uchawi na kinachoonekana katika video hiyo kichukuliwe kama sanaa tu na sio imani za kichawi.

Itazame video hiyo hapa chini;

Msemaji wa serikali awataka TUCTA kuacha siasa
Serikali yasitisha mnada wa Tanzanite