Baada ya kimya kirefu kutawala kwa mwanamuziki wa bongo fleva mwenye miondoko ya Hip Pop aliyefanya vizuri na nyimbo yake ya ”Too Much” pamoja na ”Muziki” Darasa sasa amekuja na ngoma yake nyingine inayoenda kwa jina la ”Kumbe”.

Darasa ni moja kati ya wasanii wachache wenye kipaji kikubwa katika uandishi wa mashairi na uimbaji, baada ya kimya kirefu wengi waliibua maneno mbalimbali juu ya Darasa wakidai kuwa amejiingiza katika madawa ya kulevya, lakini alipotafutwa na kuhojiwa Darasa amekuwa mtu wa kukanusha tuhuma hizo.

Kibwagizo cha wimbo wake mpya kinasema ”Kumbe maji mara moja kama maharage ya Mbeya” mashabiki wa msanii huyu dondosha maoni yako hapa chini utueleze unaelewa nini juu ya mstari huu #mawazo huru.

Katika kuthibitisha kuwa yupo fiti ameachia ngoma yake mpya ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inaongoza kwa kusikilizwa zaidi na amekata kiu cha mashabiki wake, kuusikiliza bonyeza kitufe hapo chini.

Rekodi nyingine kuandikwa leo Yanga VS Simba
Askofu Malasusa na wengine 2 watengwa na kanisa la KKKT