Kampuni ya DataVision International imetoa siri kubwa ya mafanikio ambapo imepania kuikomboa jamii kwa kutoa elimu mbalimbali kuhusu namna ya kuweza kujikwamua na kuongeza kipato.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Geofrey Mwaijonga alipokua akifungua maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo.
Amesema kuwa Kampuni hiyo mwaka huu imekusudia kujenga madarasa kwa ajiri ya kutoa elimu kwa ajiri ya watoto wa kike ambao wanakuwa wamepoteza ndugu zao kutokana na changamoto mbalimbali za maisha.
“Katika maadhimisho haya ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya DataVision International, tumepanga kutembelea na kushiriki katika vituo vya watoto yatima mbalimbali na kingine ni kujenga madarasa ya Kompyuta ambayo yatawasaidia wasichana na wale wasiojiweza,”amesema Mkurugenzi wa DataVision International, Geofrey Mwaijonga
-
Mamba avamia hospitali, ahusishwa na ushirikina
-
Kamanda aahidi ukilema kwa watakaoandamana Aprili 26
-
Dkt Tulia: Sina uhakika kama ‘Mange’ ni binadamu wa kawaida