Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Tano Mwera amewaarika watu binafsi na mashirika mbalimbali kuwekeza katika Wilaya yake ya Busega katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuweza kujiongezea kipato kupitia wilaya hiyo iliyojaa kila aina ya hitaji la mtanzania.

Busega ni miongoni mwa Wilaya zilizozungukwa na raslimali za kutosha hapa nchini, hivyo ni wakati mwafaka kwa wawekezaji kuwekeza katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

“Wilaya hii ina kila sababu ya kuwa na wawekezaji wa aina zote kutokana na jografia yake ikiwemo kuzungukwa na ziwa Victoria, barabara kuu ya kwenda Afrika mashariki, ardhi ya kutosha na yenye kukubali kila zao, ulinzi wa kutosha na wananchi wenye kujituma katika kufanya kazi” amesema Mwera.


Video: Jerry Murro aondoka na mwananchi aliyemjibu ‘Labda uje na Rais’ | Msinijaribu nawaambia

FC Barcelona, Atletico Madrid waishutumu FIFA
Video: Jinamizi ajali lazidi kutikisa, JPM ahitimisha kilio cha miaka 22