Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amewataka wananchi wa wilaya hiyo wanaoishi mabondeni kuhama ili kuweza kuepuka majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza wakati mvua zinapoanza kunyesha.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea wahanga wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni mara baada ya mvua kubwa kunyesha mfululizo niliyosababisha madhara makubwa kwa jamii.

“Niwasihi tu wananchi mnaoishi huku mhame ili kuweza kuepukana na majanga kama haya, ni bora kujikinga kabla ya kutokea kwa maafa mengine, ni uharibifu mkubwa uliotokea,”amesema Hapi

Aliyesambaza Ukimwi kwa makusudi afungwa jela miaka 24
Video: Itazame 'Mans Not Hot' ya Big Shaq