Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, Theresia Mahongo amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya uwepo wa mitandao ya simu za mkononi kupashana habari za maendeleo na kufanya biashara salama kupitia huduma za fedha za mitandao hiyo, badala ya kuhamasishana vitendo vya kihalifu.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wilayani humo, ambapo amesema kuwa kumekuwepo na tatizo la matumizi mabaya ya simu za mkononi jambo ambalo linapaswa kukemewa ili mitandao hiyo iweze kuchangia maendeleo.
Aidha, katika uzinduzi huo, wakazi wa wilaya ya Karatu na mkoa wa Arusha kwa ujumla wamejitokeza kushuhudia uzinduzi wa duka la kampuni ya simu za mkononi ya Airtel linalotarajiwa kusogeza huduma zake kwa wakazi hao.
Kwa upande wake, Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara, Polas Emmanuel amesema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo ni utekelezaji wa mpango wa kampuni yao wa kusogeza huduma kwa jamii nchi nzima.(PAUSE)
-
Sugu, Masonga waachiwa huru
-
Heche akerwa na serikali ya CCM aitaka iwe sikivu
-
Sababu ya Sugu kuachiwa huru yaanikwa
Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wa huduma za Airtel wamesema watapata urahisi katika shughuli zao ikiwemo mawasiliano ya simu na miamala ya kifedha yakuweka pamoja na kutuma.(PAUSE).