Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amemuagiza afisa elimu wa wilaya ya Ilala kuhakikisha kila shule inafanya uandikishaji wa wanafunzi kwa ajili ya mafunzo ya vikundi vya skauti.
Mjema ameyasema hayo hii leo katika maadhimisha ya miaka 100 ya skauti tangu kuanzishwa kwake 1917 sambambana kuzindua wiki ya mawasiliano ya anga kwa njia ya upepo.
“Ikama ya walimu wa skauti ni ndogo natoa agzio kwa afisa elimu kufanya uandikishaji wa skauti wakike na wakiume katika kila shule na kuhakikisha kila shule kunakuwa na mwalimu mmoja ambaye atakuwa anawafundisha skauti hao,” amesema Mjema
Aidha, ametoa wito kwa watoto na skauti wote pindi wanapoona matukio ya kidhalilishaji au kufanyiwa watoe taarifa kwa mamlaka husika kwani serikali ipo kwa ajili yao na itawalinda.