Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa tar 1 mwezi wa nne ni siku ya kupanda miti katika Wilaya hiyo.

Amesema kuwa miti inafaida kubwa katika mazingira ya binadamu na wanyama pia katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

Aidha, amesema lengo la upandaji miti ni kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamekuwa yakitokea sehemu mbalimbali nchini.

“Wananchi kila mmoja ana wajibu wa kutunza miti yetu kwani ndiyo inayotuingizia kipato kutoka kwa watalii wa nje ya nchi,”amesema Mjema.

 

Shy-rose alalama, asema haki haijatendeka kukatwa jina lake
#Hapokale