Bingwa wa masumbwi katika uzito wa WBC, Deontay Wilder amesema kuwa atampiga Anthony Joshua nyumbani kwake Uingereza.

Wilder mwenye umri wa miaka 32 alitetea taji la mkanda wa WBA na IBF kwa kwa kumpiga Bermaine Stiverne kwa KO (Knock Out) na baada ya pambano hilo alisema anataka kupambana na Anthony Joshua.

”Kama Joshua ndio bora, na bingwa , Waingereza wanatakiwa kumwambia ajitokeze na apigane na mimi ndio mujue kwamba yeye ndio bora. Moyo wangu unaniambia kwamba mimi ndio bora na kama sio bora basi ningependa aliye bora aje anionyeshe,” alisema Deontay Wilder.

Tazama hapa chini jinsi Wilder alivyomshushia kipigo Bermaine Stiverne na alichosema kuhusu Anthony Joshua;

Majaliwa apiga marufuku Mawaziri kutoa matamko
Nchemba: Wapinzani hawakupaswa kusimamisha wagombea