Msanii anayeiwakilisha vizuri Tanzania na muziki wa Bongo Fleva kimataifa, ambaye ni Rais wa kundi la WCB, Diamond Platinumz ameachia ngoma zake mbili kwa mpigo moja ikienda kwa jina la sikomi nyingine ikienda kwa jina la niache amefanya muziki huo bila kumshirikisha msanii yeyote huku akizungumzia maisha yake.

Katika nyimbo hizo Diamond amedhihirisha kipaji chake cha uandishi ambapo ameonekana kutumia ustadi wa hali juu kunogesha nyimbo kwa kutumia baadhi ya methali na nahau zilizoakisi maisha yake na stori zake ambazo zilitikisa katika mitandao ya jamii.

Katika muziki huo amewataja baadhi ya wapenzi aliowai kutoka nao, akiwemo Wema Sepeto, Penny na Zarina Hassan ambapo ameeleza baadhi ya vimbwanga alivyopitia pindi alipokuwa na wapenzi hao.

Mashabiki wa Diamond Platinumz wametafsiri wimbo huo kwa namna nyingi, huku wengine wakisema kuwa nyimbo hizo amezitoa maalumu kwa mpenzi wake wa sasa Zarina, huku wengine wakisema alichoimba Diamond ni kuhusu maisha yake akimuongelea Adbdul Naseeb na Diamond Platinumz.

Kusikiliza nyimbo hizo mbili bonyeza link hapa chini kisha toa maoni yako.

 

Maaskofu watoa ya moyoni kuhusu Rais
Video: Mama Samia alivyotinga hospitali kumuona Lissu, Moto zaidi wawaka rushwa boss Takukuru