Daktari Bingwa wa upasuaji wa Magonjwa ya Mgongo wazi na Vichwa vikubwa, Nicephorus Rutabasibwa kutoka Taasisi ya mifupa MOI amesema kuwa magonjwa hayo husababibishwa na uumbaji wakati mtoto akiwa tumboni.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa hali hiyo hutokea siku za mwanzoni mwa uumbaji wakati mtoto akiwa tumboni.
Amesema kuwa hilo ni tatizo la kuzaliwa na hutokea mwanzoni kabisa mwa uumbaji, hivyo kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo hilo.
“Sisi huwa tunashauri akina mama walio katika umri wa kuzaa kula vyakula ambavyo, vitasaidia kujenga na kuimarisha afya pindi wanapokuwa wajawazito,”amesema Dkt.