Baraza la tiba asili na tiba mbadala leo Julai 12 2016 limetangaza kuwafutia usajili Matabibu 3 nawengine 4 kupewa onyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa baraza hilo Dkt. Edmond Kayombo  amezitaja sababu za kuwafungia Matabitbu hao kuwa ni kukiuka sheria ya Tiba asili na Mbadala pia wamekiuka tamko la Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto, Ummy Mwalimu.

Matabibu waliofutiwa usajili ni

  1. Fadhil Kabujanja wa kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic
  2. Juma Mwaka wa kituo cha Foreplan Clinic
  3. Abdallah Mandai wa kituo cha Mandai Herbal Clinic

Matabibu waliopewa onyo

  1. Simon Rusigwa wa kituo cha Sigwa Herbal Clinic
  2. John Lupimo wa kituo cha Lupimo Sanitarium Clinic
  3. Castory Ndulu wa kituo cha  Ndulu Herbal Clinic
  4. Esbon Baroshigwa wa kituo cha Aman Herbal Clinic

Waziri wa Afya Atumbuliwa, Rwanda
Naibu Waziri Mpina Atoa Mwezi Mmoja kwa kiwanda Cha Twiga Cement Kurekesha Miundo Mbinu