Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kampuni ya DataVision International kwa kuanzisha mradi wa utambuzi wa sanaa za ufundi Tanzania na kuwaunganisha wasanii.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo ulioandaliwa na Kampuni ya DataVision iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni kubwa sana iliyofanywa na Kampuni hiyo.

Amesema kuwa makampuni mengine yanatakiwa kuiga mfano wa DataVision ili kuweza kuwakomboa wasanii wa Tanzania ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi katika sanaa na kutaka kujikwamua na umasikini.

“Mimi nawapongeza sana Kampuni ya DataVision kwa hatua hii, wamefanya kazi kubwa sana kuweza kuwaunganisha wasanii na kuanzisha mradi huu,serikali itauangalia mradi kwa kaeribu sana,”amesema Dkt. Mwakyembe

Video: Zari afanya kufuru Mlimani City
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 15, 2017