Dkt. Louis Shika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kutangaza dau kununua nyumba tatu za mfanyabiashara Said Lugumi kwa shilingi bilioni 3.2 zilizokuwa zikipigwa mnada na kampuni ya Yono lakini akashindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo, ameanza mchakato wa kurejesha fedha zake zilizopo nje ya nchi.

Amesema kuwa leo jumamosi amelipa Dola 100 za Kimarekani sawa na shilingi (220,000) za Kitanzania kwa ajili ya bima ili aweze kutumiwa fedha zake nchini.

Dkt. Shika amesema hayo mara baada ya kukutana na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alipokuwa ametembelea Shirika la Posta kuzungumza na wafanyakazi, walimkuta Dkt. Shika akiwa katika shirika hilo, na kudai kuwa yupo hapo kwa ajili ya malipo.

“Nimelipa dola 100 za bima ili kukamilisha fedha zangu zije na nilipie zile nyumba, hili la bima lilikuwa ni muhimu sana kwangu,”amesema Dkt. Shika

Hata hivyo, nyumba moja ilishauzwa kwa mhindi aliyeshika namba mbili katika mnada huo huku kampuni ya Yono ikisema itaendelea na mnada wa kuziuza nyumba zingine zilizobaki.

 

Wachina wakamatwa jijini Dar es salaam
Halmashauri zapigwa marufuku kuingia makubaliano na NGO's