Watayarishaji wa series maarufu ya muziki ya ‘Empire’ iliyoteka vichwa vya burudani mwaka huu, wameachia trailer ya kwanza ya msimu wa pili.

Trailer hiyo inaonesha vita nzito ya familia ya Lucious Lyon (Terrence Howard) ambaye kwenye msimu wa kwanza aliishia jela. Cookie (Taraj P. Henson) anamtembelea Lucious Lyon jela akijidai anaenda kumsalimia kwa mema huku akiwa na lengo baya nyuma yake.

Kijana mkubwa wa Lucious, Andre (Trai Byers) anapanga kumnyang’anya baba yake kampuni ili awe Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Empire Entertainment. Wakati Lucious alimuacha mtoto wake wa pili Jamal (Jussie Smollett) kuwa mmiliki wa muda wa kampuni, uhusiano wa mtoto huyo na mama yake unayumba na wanakuwa maadui wakubwa.

Wakati huohuo, uadui kati ya vijana wa Lucious Lyon wenye vipaji vikubwa katika muziki unazidi kujengeka. Jamal anasikika akimwambia mdogo wake (Hakeem), “nitaizika album yako”. Hakeem anamjibu, “nitakuwa mkubwa zaidi yako, mkubwa zaidi ya baba pia.”
 

Ni vita ya familia iliyosota kwenye muziki na kutengeneza kampuni kubwa ya muziki. Mafanikio ya kampuni hiyo yamegeuka kuwa chanzo kikubwa cha vita kati yao, nani amiliki kampuni?

Msimu wa pili utazinduliwa rasmi Septemba 23 mwaka huu, kwenye kituo cha runinga cha FOX. Mastaa wengi wanatarajiwa kuwa wageni waalikwa akiwemo Pitbull ambaye ataonekana kwenye series hiyo akiimba wimbo wake ‘”No Doubt About It” akiwa na Jamal.
Baada ya uzinduzi huo, watanzania pia tutapata nafasi ya kuiona kwa kuipakuwa kwenye mtandao.

Ligi Ya Mabingwa Ulaya, Man Utd Wapangiwa Vibonde
Mambo Magumu Chelsea, Salah Arejeshwa Italia