Kwa utaratibu uliopo huku Indonesia ni kwamba mwanamke akifiwa na mtu wake wa karibu, mume, watoto au wazazi hutakiwa kukatwa kidole chake cha mkononi na kukizika pamoja na mpendwa wake aliyetangulia mbele za haki.
Hivyo endapo atafiwa na mtu moja basi kidole chake kimoja kitakatwa na kuzikwa na kadhalika, utaratibu huu ni ishara ya kuonyesha hisia kali na upendo wa hali ya juu alionao kwa mtu wake aliyefariki dunia.
Na hii haijalishi katika familia ameondokewa na watu wangapi, kwani kila atakayetangulia mbele za haki mwanamke katika familia hukatwa kidole chake na kuzikwa pamoja na maiti hiyo.
Ni utamaduni wa kushangaza kidogo lakini ndivyo ambavyo ilikuwa ikifanyika kwa imani zao kwa watu wa Indonesia kabila la dani, kwa sasa serikali ya nchi hiyo imepiga marufuku kutekeleza utamaduni huo ikidai kuwa ni kuvunja haki za binadamu.