Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu leo imetoa msimamo wake kuhusu jeshi la polisi na kusema kuwa hawaoni jitihada zozote kutoka kwenye jeshi hilo kuchunguza jaribio la mauaji ambalo ndugu yao lilimpata Septemba 7, 2017.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es Salaam na Kaka wa Mbunge huyo, Alute Mughwai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  ambapo amehoji kitendo cha polisi kutokumfuata dereva wa Lissu jijini Nairobi badala yake wanamsubiri Dar es Salaam.

“Yule kijana kwenye picha ukimwona yuko vizuri tu, sasa wanaposema anapata huduma ya kisaikolojia wakati kwenye magazeti anaonekana hii inatupa changamoto. Ndugu zangu, mheshimiwa Lissu amepigwa risasi na watu tunaowatafuta, huyo kijana aje. Kuja kwake kutatusaidia kupata majibu ya mambo mengi,”amesema Mughwai

 

Video: Rado aachia filamu mpya, aeleza Diamond alivyotaka pesa nyingi kushiriki
Facebook kuonyesha ligi ya Uingereza?