Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ni lazima kutekeleza masuala mbalimbali aliyoyaahidi Watanzania wakati akiingia madarakani mwaka 2015, ambayo yanalenga kuwaletea wananchi maendeleo.

Wakati alipokuwa akizindua mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema kuwa aliamua kutimiza ahadi ya Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1973 ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

Rais Magufuli alisema “Nataka yote tuliyoyaahidi tuyatekeleze, nataka ofisi hizi nzuri tulizojenga ziwe na watu, na zianze kutoa huduma kwa wananchi”.

Alisisitiza, “Jukumu langu lilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere, na  nilipata nguvu baada ya kukumbuka kuwa ziko nchi nyingi tu duniani ikiwemo nchi za Afrika kama Nigeria na Cote d’Ivoire ambazo zilihamisha makao makuu  ya nchi yao katika kipindi kifupi, nataka kuwahakikishia na mimi nakuja Dodoma kwa sababu hakuna kinachonichelewesha”.

Rais TFF aihofia Senegal, asema hana shaka na Algeria, Kenya
Video: Serikali kukamilisha ujenzi wa barabra ya bilioni 500 Dodoma