Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu sasa imezidi kuimarika na kusema atasafirishwa kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo ambapo amesema kuwa mpaka sasa mbgunge huyo anaendelea vizuri na kudai kuwa amefanyiwa upasuaji mara 17.

“Tundu Lissu mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mara 17 amewekewa damu nyingi kuliko mgonjwa yoyote katika hospitali ya Nairobi lakini Mungu ameendelea kutenda miujiza kwake, saizi mashine zote zilizokuwa zinamsaidia zimeondolewa, saizi hapumulii mashine tena, mirija yote aliyokuwa anatumia kwa ajili ya chakula imeondolewa na juzi kwa mara ya kwanza aliweza kukaa,”amesema Mbowe.

Hata hivyo, ameongeza kuwa serikali inafahamu watu ambao wameshambulia Tundu Lissu na kudai wao hawana imani na vyombo vya dola nchini na kusema vyombo hivyo vimekuwa tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hawana nia ya dhati katika kufanya uchunguzi juu ya sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi mnamo Septemba 7, 2017

 

Nicki Minaj aeleza alichowaandalia mashabiki wake
Wanawake 28 wahitimu kozi ya ukocha TFF