Mbunge Jimbo la Kawe lililopo jijini Dar es salaam, Halima Mdee amesema kuwa halmashauri zote zimenyang’anywa mamlaka ya kutengeneza barabara nchini hivyo wananchi wanatakiwa kulifahamu hilo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha Halmashauri ya jiji kilichojumuisha wabunge na madiwani kwaajili ya kujadili mipango kazi ya jiji hilo.

Amsema kuwa kwa sasa wananchi wanatakiwa watambue kuwa barabara zote haziko chini ya halmashauri hivyo kimeundwa chombo kingine ambacho kitakuwa maalum kwaajili ya kushughulikia barabara.

“Kwa sasa mambo yamebadilika tofauti na mwanzo, kuna chombo maalumu kilicvhoundwa kwaajili ya kushughulikia barabara hizi, lakini nashindwa kuelewa kuwa hawa watu watawajibishwa na nani endapo wataenda kinyume na sheria,” amesema Mdee.

Hata hivo ameongeza kuwa kabla ya chombo hicho kuundwa halmashauri zilikuwa zikisimamia barabara vizuri, hata pale mkandarasi alipaenda kinyume aliweza kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

 

Mkemia Mkuu awanyooshea kidole mawakala wa forodha
Madee amuomba radhi Jackline Wolper