Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Harry Kane amepiga hat-trick ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa Ulaya na kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Apoel Nicosia.

Kane alianza kufunga bao la kwanza katika dakika ya 39 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Toby Alderweireld kabla ya kupachika bao la pili dakika ya 62 na bao la tatu dakika ya 67.

Ushindi huo umeifanya Tottenham kufikisha pointi 6 ikiwa nafasi ya pili kundi H baada ya kucheza michezo miwili sawa na Real Madrid yenye pointi 6 pia zikitofautiana kwa magoli wakati timu za Borrusia Dortimund na Apoel Nicosia zikisalia bila pointi.

Tazama mabao aliyofunga Harry Kane hapa chini;

Mugabe amchimba mkwara mwingine Trump kuhusu Jeshi
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 27, 2017