Harry Kane amefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0 ambao klabu ya Tottenham imeupata dhidi ya Huddersfield.

Kane alitangulia kuipatia Tottenham bao la kuongoza dakika ya 9 kabla ya Ben Davies kupachika bao la pili dakika ya 16 kisha Kane akafunga bao la tatu dakika ya 23, Moussa Sissoko alipiga bao la nne dakika ya 90 na kuifanya Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Huddersfield.

Kwa ushindi huo Tottenham imefikisha pointi 14 ikiwa katika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo saba.

Tazama magoli ya mchezo huo katika video hii hapa chini;

Marekani na China kuijadili Korea Kaskazini
Janjaro azungumzia mpango wa kutaka kujiunga na ‘Weusi’