Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema kuwa wanaendelea na upelelezi juu ya taarifa ya kutekwa kwa Ben Saanane na kudai hawawezi kusema kila hatua wanayochukua.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari, Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia.

“Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu imeshafanyika,”amesema Boaz.

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 21, 2017
NEC: Hakuna chama kilichojitoa kwenye mchakato wa uchaguzi