Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Majura Musiba ametaja orodha ya watu hatari kumi katika usalama wa taifa ambao wanatakiwa kushughulikiwa na vyombo vya usalama kabla hawajaleta madhara kwa jamii.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa watu hao wamekuwa wakiratibu mambo mbalimbali kwa ajili ya kuhatarisha amani ya nchi.
Amesema kuwa usalama wa taifa ni muhimu kushinda vyote, hivyo kuchezea amani kwa manufaa ya watu flani wachache haikubariki hata kidogo.
Aidha, amewataja watu hao kuwa ni pamoja na, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mange Kimambi, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Julius Mtatiro, John Heche, Maria Sarungi, John Marwa, Evalist Chahari,
“Watu hawa ni hatari na wanapaswa kushughulikiwa mara moja kabla mambo hayaja haribika, kwani tukiwaachia hawa watu hawana nia nzuri hata kidogo, lengo la hawa ni kuvuruga amani si vingine,”amesema Musiba