Daktari wa magonjwa ya Akili, Saidi Kuganda kutoka hospitali ya Muhimbili amezungumza kinagaubaga suala zima la msongo wa mawazo pamoja na Sonona ambapo amesema kuwa kwa kiasi kikubwa hupelekea mtu kujiua, upofu au kupata kiharusi (Stroke).
”Msongo wa mawazo sio ugonjwa, ni mawazo yamesongamana lakini kinachofuatia pale unaweza ukawa sawa au mgonjwa lakini kuna maradhi yanayohusiana na msongo wa mawazo mfano wasiwasi sana au maradhi ambayo yanatokana na mshtuko” amesema Daktari Saidi.
Utafiti uliofanywa na MUHAS 2018 na kuchapishwa rasmi mwaka huu umeonyesha kuwa tofauti na ilivyokuwa zamani kuwa wazee ndio wanapata ugonjwa wa kiharusi zaidi, lakini hivi sasa idadi ya vijana wa kitanzania wanaopata kiharusi inapanda.
Chanzo kimetajwa kuwa ni msongo wa mawazo unaopelekea Presha.
Zipo namna nyingi ambazo vijana wengi hutumia kupungumza msongo wa mawazo zinaweza kuwa sahihi au ambazo si sahihi.
Daktari wa akili amefanunua zaidi kuhusu msongo wa mawazo, sonana na kufahamu madhara yake.