Kufuatia zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotolewa na Serikali kwa wananchi wote wa Tanzinia bara, tayari sheria inayosimamia zuio hilo imetolewa, iliyotungwa kwa mujibu wa kifungu namba 230(2) (f) cha sheria inayohusika na usimamizi wa mazingira.
Sheria hiyo ndogo imeainisha makosa matano ambayo ni kuzalisha na kuagiza mifuko ya plastiki, kusafirisha nje ya nchi mifuko ya plastiki, Kuhifadhi na kusambaza mifuko ya plastiki, kuuza mifuko ya plastiki na kosa la mwisho ni kumiliki na kutumia mifuko ya plastiki pamoja na adhabu zake…,Bofya hapa kujua zaidi undani wa sheria hii