Mshambuliaji Romelu Lukaku alifunga bao dhidi ya timu yake ya zamani katika mchezo ambao Manchester United waliichapa Everton mabao maanne kwa sifuri katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa jana.

Man Utd ilipata bao la kuongoza katika dakika ya nne kupitia kwa Antonio Valencia baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na Nemanja Matic na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku mabao ya Man Utd yakipaitikana dakika za lala salama baada yaHenrikh Mkhitaryan kuipatia bao Man Utd kabla ya Lukaku na Anthony Matrial kufunga mabao mengine mawili.

Katika mchezo huo mshambuliaji Wyne Rooney alikuwa akirejea katika uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na Everton msimu huu na mashabiki walionekana kumpokea kwa heshima ya kipekee.

Tazama video ya magoli yaliyofungwa na Man Utd dhidi ya Everton hapa chini;

Yanga mlikosea kumuita 'Okwi' Muhenga- Manara
Bob Junior atoa siri ya kushindwa kufanya vizuri kimuziki