Wasanii wa muziki wa Bongo fleva nchini, Ommy Dimpoz na Harmonize siku za hivi karibuni wameachia ngoma zao mpya ambazo zinafanya vizuri wakiwa wamewashirikisha wasanii toka nje ya Tanzania.
Ommy Dimpoz ameachia ngoma yake inayoenda kwa jina la Yanje ambayo amefanya na msanii toka Nigeria anayejulikana kwa jina la Sey Shay ambapo tangu kuachiwa kwa ngoma hiyo inafanya vizuri katika mtandao wa You Tube na kushika nafasi ya 15 kati ya video zinazoongozwa kwa kutazamwa.
Video hiyo imeachiwa rasmi siku ya jana, Mei mosi, na tayari imekwisha tazama na watu 39,716.
Yanje ni moja ya nyimbo ya Ommy Dimpoz itakayofanya vizuri kutokana na mchanganyiko wa lugha zilizotumika katika wimbo huo, ambapo lugha tatu zimetumika ikiwa ni lugha ya Rwandese, Kiswahili na kingereza.
Bonyeza kitufe hapo chini kuutazama wimbo huo na kutuandikia wimbo gani unaukubali kuanzia mistari, video na collabo ipi imefanya vizuri.
Kwa upande wa Harmonize yeye amefanya kibao chake na msanii wa Hip Pop toka Ghana anayejulikana kwa jina la Sarkodie ambaye ni moja ya wasanii wakubwa nchini Ghana wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki mpaka kushindanishwa katika tuzo mbalimbali ikiwemo ya BET, na kwa mwaka 2012 Sorkodie aliweza kushinda tuzo ya Msanii bora wa Kimataifa katika tuzo za BET Afrika.
Harmonize ameachia ngoma yake na Sorkodie inayoenda kwa jina la ”DM Chick” nayo inafanya vizuri katika chat za Youtube na kutazamwa na watu wengi zaidi tangu kuachiwa kwa ngoma hiyo tarehe 30 April mwaka huu.
Bonyeza kitufe hapo chini kuutaza wimbo huo na tuandikie wimbo gani unaukubali.