Mchekeshaji Michael Dapaah maarufu kama Big Shaq kutoka Uingereza amabye hivi karibuni amejipatia umaarufu mkubwa na kuanza kufatiliwa katika mitandao ya kijamii hasa baada ya kutoa ‘freestyle’ kwenye radio ya BBC katika kipindi cha ‘Booth Rap Show’ hatimaye ameachia rasmi video yake ya ngoma inayoitwa ‘Mans Not Hot’.

Big Shaq amejipatia umaarufu kutokana na mtindo wake wa kurap ambao unachekesha sana na umewavutia watu wengi duniani.

Video hiyo imefanyika mjini Miami Marekani huku ikiwahusisha baadhi ya watu maarufu kama vile Jim Jones, Waka Flocka, Lil Yatchy, Snoochie Shy na legendary DJ Khaled chini muongozaji wa video Marv Brown.

Itazame video hiyo hapa chini;

Video: DC Hapi awataka wanaoishi mabondeni wahame
Mpina: Nitang'atuka nafasi ya Uwaziri kama nitashindwa