Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul makonda leo ameonyesha picha za jengo kubwa la hospitali ya kinamama ambalo ujenzi wake tayari umeanza kwa msaada kutoka Serikali ya Korea Kusini na linatarajiwa kuzinduliwa na Raais Magufuli mwezi wa nne mwakani.

Jengo hilo litakalogharimu jumla ya shilingi bilioni 8 na milioni 800 litakuwa na uwezo kulaza wakinamama(wagonjwa) 160 kwa wakati mmoja na litakuwa na chuo kwaajili ya wanafunzi na tayari Madaktari kutoka Korea wamesha anzaa kutoa mafunzo ya magonjwa ya kinamama. Bofya hapa kutazama video kufahamu zaidi:-

Muziki: Higher Live Version - Nikki wa Pili, produced by Dj D-Ommy
Kamanda Sirro azungumzia undani wa tukio la Majambazi kuua Polisi wanne Dar