Jengo la Tanesco lililopo Ubungo jijini Dar es salaam limeanza kuvunjwa ili kutekeleza agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ili kupisha ujenzi wa barabara za juu.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa baadhi ya wafanyakazi wameshaanza kuhamia katika ofisi mbalimbali zilizopo jijini Dar es salaam, huku akiongeza kuwa taratibu na wengine wataendelea na zoezi hilo.

“Kama mnavyojionea ninyi wenyewe tayari zoezi limeshaanza la kubomoa jengo, ukiangalia ukuta huu wa mbele umeshabomolewa tayari,”amesema Muhaji

Video: Mpina atangaza vita dhidi ya uvuvi haramu
Sakaya: Bora kustaafu siasa kuliko kuhama chama