Msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro ametangaza kurudi kazini rasmi baada ya rikizo yake kumalizika, akiongea na waandishi wa habari leo 05/08/2016 amesema anasubiri nakala ya hukumu kutoka TFF kwani tayari amerudi hivyo wampelekee nakala hiyo ofisini kwake kwasababu yeye ndiyo mhusika.

Muro amesema hayo kufuatia TFF kumfungia mwaka mmoja kutokujihusisha na soka pamoja na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tatu ndani ya siku 90 baada ya kukutwa na hatia ya kuisema vibaya TFF katika vyombo vya habari ambapo kamati ya maadili ya TFF imetoa nafasi kwa Jerry Muro kukata rufaa kama watakuwa hawajaridhishwa na maamuzi ambayo yametolewa. Bofya hapa kusikia alichokisema Jerry Muro  #USIPITWE

Kigwangala Afanya ziara Ya Kushtukiza Kituo Cha Tiba Asili Foreplan (T) Limited
Dawasco Waikacha Ziara Ya Naibu Waziri Wa Mazingira Mh.Mpina