Aliyekuwa Msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha porojo na badala yake wajikite katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amewataka viongozi wa Chadema wanaodai kuwa wanafuatiliwa na watu ili wawauwe wawataje hadharani.

“Nimemsikia baadhi ya wabunge wa Chadema wakisema kuna watu wanawafuatilia, Dada yangu kule Bunda (Ester Bulaya) akisema anafuatiliwa na watu waliovaa kininja, nani awafuatilie nyie? amehoji Muro.

Aidha, Muro amemtaka Lema kuacha mara moja kumfuatilia bali aendelee na kazi yake ya ubunge na si kupoteza muda mwingi kwaajili ya mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kwani hayatamsaidia.

Hata hivyo, Murro amekanusha tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwa anajipendekeza kwa Rais Dkt. Magufuli ili aweze kuteuliwa kwa nafasi yeyote serikalini.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 8, 2017
Bayern Munich yamrejesha Jupp Heynckes