Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro mapema leo hii ameapishwa na kuanza kazi rasmi katika nafasi aliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Mara baada ya kula kiapo Muro amewaagiza Wakurugenzi pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ndani ya wiki mbili kuandaa taarifa za 10%ya Mikopo ya vijana na wanawake.
Muro amesema wananchi wa Wilaya yake ni shupavu ila wanahitaji hamasa hivyo ameomba muda mchache kuleta mabadiliko katika wilaya hiyo.
”Nipe muda mchache Tanzania itajua Afrika itajua” amesema Muro mara baada ya kula kiapo.