Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuua majambazi watatu, katika majibizano ya risasi yaliyotokea eneo la Mbagala Kiburugwa Agosti 29, 2018 majira ya saa 1:00 Usiku.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lazaro Mambosasa,ambapo amesema kuwa majambazi hao walikuwa kwenye mikakati ya kufanya wizi katika maeneo hayo ndipo askari waliokuwa doria wakawakurupusha na kuanza kurushiana risasi.

”Majambazi walikuwa watano, walijaribu kurushiana risasi na askari wetu ambapo walijeruhiwa watatu na wawili walifanikiwa kutoroka lakini majeruhi ambao wote ni wanaume walifariki wakiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili”, amesema Mambosasa

 

 

Taifa Stars kuifuata Uganda kesho
EXCLUSIVE: Tazama Betty Barongo akichambua mistari ya wimbo wake “Prisoner no more”