Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wale wote waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati mbili za uchunguzi za bunge zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kujisalimisha wenyewe kwenye Ofisi za Mkurugenzi wa Upelezi wa Mashtaka ya Jinai ili kuhojiwa.

Ameyaema hayo hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare es salaam, ambapo amesema kuwa hakuna haja ya kuwafuata na kuwakamata bali wanatakiwa kuripoti kwa hiari yao.

“Nawaomba wale wote waliotajwa katika kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa hiyo niwaombe waanze kujisalimisha wenyewe kabla ya kuwafuata katika hilo,”amesema Sirro

Video: IGP Sirro awatoa wasiwasi wazazi, anena mazito kuhusu Lissu
Familia yamrejesha Bony Swansea City