Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewahutubia wakazi wa Magomeni kufuatia ziara aliyoifanya kwa wakazi hao ambao nyumba walizokuwa wakiishi katika eneo hilo zilivunjwa mwaka 2012 kwa makubaliano ya kujengwa nyumba za kisasa lakini kwa takribani miaka mitano nyumba hizo hazikujengwa hali ambayo iliwafanya wakazi hao waishi maisha ya kuhangaika.

Kufuatia hali hiyo, Rais Magufuli amewaeleza wananchi kile kilichokuwa kikiendelea na ameonyesha kukerwa na vitendo hivyo vya baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu kuwanyima haki wanyonge. Amesema vitendo hivyo vya unyanyasaji viishe mara moja na watanzania wakae kwenye nchi yao kwa amani. Bofya hapa kutazama video

Safari Ya Urusi 2018: Brazil Yachanja Mbuga
Joto La Pambano La Leo, Masau Bwire Aamikia Uwanja Wa Uhuru