Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa ambao amewateua na kuwataka wakafanye kazi kwa juhudi na weledi.

Hafla ya uapisho huo imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Jaji Mkuu  Ibrahim Hamis Juma , Spika wa Bunge Job Ndugai na wengineo.

“Nyinyi ni wawakilishi wa Watanzania, mkawe watumishi wao, mkawe sauti yao, mkamtangulize Mungu, wakuu wa mikoa mkaangalie kuna vitu gani ambavyo mnaweza kufanya katika kubadilisha uchumi wa eneo lake, wote mlioteuliwa sitaki nisikie mtu anasema yeye mgeni, tunataka maeneo yenu muyajue. Najua mkitoka hapa wengine mtakwenda kusherehekea wengine mtakwenda kupewa pole, mkafanye kazi,” amesema Rais Dkt. Magufuli.

Hata hvyo, Rais Dkt. Magufuli amefanya mabadiliko kwa mkuu mpya wa mkoa wa Dodoma, Christine Mndeme na kumpeleka mkoani Ruvuma, na yule ambaye alikuwa mkoani Ruvuma, Binilith Mahenge  kutakiwa kwenda kuripoti mkoani Dodoma mara moja.

Spurs kuikabiri Man United bila Harry Kane
Prof. Elisante awaaga watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo