Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu amesema kuwa kama ikibainika kuwa ni kweli askari wa kikosi cha usalama barabarani amepokea rushwa basi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa yeye binafsi hajaiona video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha askari wa usalama barabarani akipokea rushwa.
Amesema kuwa kama ikibainika ni kweli basi askari huyo pamoja na mtoa rushwa watashughulikiwa ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa askari huyo.
“Mimi binafsi sijaiona hiyo video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, lakini kama ntaipata na kuthibitisha kuwa ni yeye aliyepokea rushwa, sheria itachukua mkondo wake,”amesema Kamanda Musilimu