Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa ametoa wito kwa vijana kuacha ushabiki bila kuchunguza madhara yake.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa mnamo Aprili 26, 2018 Jeshi la Polisi liliwakamata vijana ambao walikuwa kwenye maandalizi ya maandamano ambayo yalihamasishwa kwa njia ya mtandao na mwanadada Mange Kimambi lakini baada ya muda mfupi alianza kuipongeza serikali.

Mambosasa amewasihi vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kuwa waangalifu ili wasije kufuata mikumbo ambayo itawasababishia madhara makubwa, huku akitolea mfano vijana waliokamatwa wakijiandaa na maandamano ya Aprili 26 ambayo yalikuwa yameratibiwa na Mange Kimambi.

“Mhamasishaji Mange Kimambi baadae akaanza kuipongeza Serikali. Mange ameendelea kuipongeza serikali nasi tunampongeza kwa kuwa amerudi kundini, amesema Mambosasa.

 

 

Video: Ammy Ninje asema yuko fiti kuwakabiri Mali
Wafahamu watu 10 wenye ushawishi mkubwa zaidi Duniani