Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu amesema kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya madereva wa magari binafsi na daladala wanaoegesha magari yao kwenye vituo vya daladala.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, hivyo mtu yeyote atakaebainika kufanya hivyo atashughulikiwa kikamilifu.
Amesema kuwa hata madereva daladala hawapaswi kuegesha bali wanatakiwa kushusha abiria na kuendelea na safari.
“Kuegesha gari binafsi au daladala kwenye kituo cha kushushia abiria ni kosa kishera, hivyo kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali,”amesema Kamanda Muslim