Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Jijini Dar es salaam, John Msumule amesema kuwa watu ambao wanaishi nchini bila utaratibu wataondoka nchini ama kwa hiari ama kwa lazima.
Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es salaam, Msumule amesema wamekamata wafanyakazi tisa na wawili wakifanikiwa kuonyesha vibali na wale wengine saba watarudishwa makwao.
Amesema kuwa wametembelea Makampuni mengi na kubaini watu wengi walioajiriwa hapa nchini hawana vibali vya kufanya kazi nchini.
Aidha, Msumule amesema kuwa wamemkata dada mmoja Mganda aliyekutwa na passpot 15 katika Hotel ya Lamada hivyo atafikishwa mahakamani na wahusika wote waliofanikisha kumwezesha kupata passpot hizo.
Hata hivyo, amesema kuwa tukio jingine ni kuhusu Kampuni ya Quality group ambao walidanganya na baada ya kubanwa walilazimika kujieleza na kupelekwa na kuwekwa chini ya ulinzi huku wakiendelea kuhojiwa.