Aliyekuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Thomas Kashililah ametenguliwa katika nafasi hiyo na Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kutenguliwa kwake kumekuja mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kutangaza baraza jipya la mawaziri hii leo Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo rais amesema kuwa katibu huyo atapangiwa kazi nyingine.

“Nimetengua uteuzi wa Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah asubiri mpaka pale atakapopangiwa kazi nyingine ambayo atakayokuwa akiifanya,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa amemteua Steven Kagagai kuwa Katibu wa Bunge, kushika nafasi ya aliyekuwa katibu wa bunge hilo Thomas Kashililah ambye atapangiwa majukumu mengie,

Hispania kuandamana kupinga kujitenga kwa Catalonia
Video: Makamba, Nchemba, Mwakyembe, wapeta baraza jipya la mawaziri