Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo November 12, 2016 ameongoza mazishi ya Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel John Sitta aliyefariki dunia Novemba 7 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.

Mazishi hayo yamefanyika Urambo, Tabora kwenye eneo la makaburi ya ukoo wa Sitta ambayo yapo takribani km 2 kutoka nyumbani kwa marehemu mzee Sitta.

Wakati akitoa salamu za mwisho mbele ya umati mkubwa uliokusanyika kusindikiza mwili wa marehemu Sitta, Waziri Mkuu amesema kuwa (akionyesha sehemu walipokuwa wakikaa nyumbani kwa maerhemu Sitta) anamkumbuka sana marehemu Sitta kwani ndiye aliyekuwa akimuandaa kuwa kiongozi imara. Wakati akiongea hayo akakumbuka kauli kutoka kwa mzee Sitta iliyopelekea kumtoa machozi na kuibua hisia kubwa kwa waombolezaji. Bofya hapa kuazama video

Chadema wamtimua kada wao aliyegombea ubunge, wadai aliuza ushindi
Video: Sitta alifanya mabadiliko makubwa kwenye kanuni za Bunge - Msekwa