Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa vyanzo vinavyotumika kuzalishia mafuta nchini vinatosheleza mahitaji kwa asilimia 30, hivyo asilimia 70 ya mafuta huagizwa kutoka nje ya nchi.
Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha taarifa ya serikali kuhusu taarifa zilizozagaa nchini kuwa kuna uhaba wa mafuta ya kupikia.
“Miezi mitatu ya mwanzo kwa mwaka huu kuanzia Januari wastani wa mafuta yaliyoingizwa ni tani 30,210.71 kwa mwezi na jumla ya akiba ya mafuta yaliyopo nchini ni wastani wa tani 68, 902, hivyo hakuna upungufu,” amesema Mwijage.